Hali ya Maisha ya wakimbizi wa ndani wa Goma nchini DRC

31 Agosti 2012

Hali ya maisha inaarifiwa kuwa duni sana katika maeneo kadhaa ya mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia mapigano yanayoripotiwa mara kwa mara kati ya Vikosi vya serikali na waasi wa M23. Ingawa mapigano yamesimama au kupunguka kiasi, wimbi kubwa la wakimbizi wa ndani waliopiga kambi kandokando na Mji wa Goma imekuwa ni kero kubwa kwa utengamano wa Jimbo la Kivu ya Kaskazini. Baada ya Mashirika ya Kiraia, sasa Kanisa limechukua nafasi ya mbele kuomba mapigano na vitisho vya mgawanyiko wa nchi vikomeshwe. ujumbe wa maaskofu unasafiri wiki hii hadi mji wa New York kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kushinikiza kumalizika kwa vita.

Muandishi wetu wa Maziwa Makuu, Ramadhani KIBUGA anaangazia hali ya maisha katika kambi za wakimbizi wa ndani wa Goma. Ungana naye.

(PKG RAMADHANI KIBUGA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud