Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwenye siku ya watu waliotoweka, familia zisaidiwe kufahamu ni nini kilichofanyika:ICRC

Kwenye siku ya watu waliotoweka, familia zisaidiwe kufahamu ni nini kilichofanyika:ICRC

Familia za watu waliotoweka kote duniani kutokana na migogoro ya silaha na hali nyingine za dharura, zinakabiliana na uchungu wa kutopata habari zozote kuwahusu watu hao.

Wakati serikali husika zina wajibu chini ya sheria ya kibinadamu ya kimataifa kufanya vyovyote vile kutambua ni nini kilichofanyika kwa wale walotoweka, bado kunahitajika kujitolea zaidi ili kuzisaidia familia za watu hao kukabiliana na ugumu wa kuwapoteza watu wao, limesema shirika la kimataifa la msalaba mwekundu, (ICRC) kwenye siku ya kimataifa ya watu waliotoweka.

Shirika hilo limesema kuwa wakati mwingine familia za watu walotoweka hupata njia ya kukabiliana na ugumu huo wa mawazo na hisia kutokana na watu wao kutoweka, hata bila msaada wowote, lakini hata ikiwa ni muda gani umepita, ni muhimu serikali zifanye kila ziwezavyo kutoa maelezo zaidi, na kuwapa usaidizi wanaohitaji kukabiliana na changamoto za kila siku ili waishi kwa heshima. Dorothea Krimitas ni msemaji wa ICRC

(DOROTHEA KRIMITAS CLIP)