Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani vikali mauaji yanayoendelea Iraq na kutaka yakomeshwe

UM walaani vikali mauaji yanayoendelea Iraq na kutaka yakomeshwe

Mtaalam maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kunyonga watu kinyume na sheria na mauaji ya kiholela, Christof  Heyns, amelaani vikali mauaji yalofanywa siku ya Jumatatu ya watu 21 nchini Iraq, wakiwemo wanawake watatu. Siku mbili baadaye, watu wengine 5 waliripotiwa kunyongwa, kufanya idadi ya watu walouawa tangu Januari 1 2012 kufika watu 96.

Bwana Heyns ameelezea kuhuzunishwa kwake kuhusu viwango vya unyongaji nchini Iraq, na kulaani hasa ule wa wiki hii, huku akielezea hofu na kustaajabishwa kwake na ripoti kuwa watu wengi zaidi bado wanakabiliwa na hatari ya kunyongwa. Ameitaka serikali ya Iraq kusitisha mara moja mauaji haya. Alice Kariuki na maelezo kamili.

(TAARIFA YA ALICE KARIUKI)