Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto ni taswira ya Mali ya matatizo ya chakula na lishe:Amos

Watoto ni taswira ya Mali ya matatizo ya chakula na lishe:Amos

Watoto ndio taswira ya matatizo ya chakula na lishe nchini Mali na eneo zima la Sahel amesema mratibu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja nwa Mataifa bi Valarie Amos baada ya nkukamilisha ziara yake nchini humo.

Bi Amos alitembelea kituo cha lishe cha Gabriel Toure mjini Bamako ambacho kinatibu watoto zaidi ya 1000 wenye matatizo ya utapia mlo tangu mwanzoni mwa mwaka.

Amesema maisha nya watoto nchini humo yameghubikwa na matatizo ya lishe ambayo yanafahamika na kuna ujuzi na uwezo wa kukabiliana nayo, ila kinachokosekana ni fedha za kufanya kila linalohitajika . Bi Amos amesema watoto takriban 150,000 nchini kote Mali wametibiwa maradhi ya utapia mlo uliokithiri katika kituo cha Gabriel Toure mwaka huu. Umoja wa Mataifa umeomba dola milioni n213 kwa ajili ya kukabiliana na mahitaji ya kibinadamu Mali lakini hadi sasa ni aslimia 46 tuu ya fedha hizo ndizo zilizopatikana.