Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Homa ya Kidingapopo iaongezeka duniani:WHO

Homa ya Kidingapopo iaongezeka duniani:WHO

Shirika la afya duniani WHO limechapisha ripoti inayoonyesha kwamba homa ya kidingapopo inaongezeka duniani. Kwa mujibu wa shirika hilo katika miongo mitano iliyopita matukio ya kuzuka kwa homa ya kidingapopo yameongezeka mara 30 .

Kumekuwa na visa vipya kati ya milioni 50 hadi 1000 vinavyokisiwa kuzuka kila mwaka katika zaidi ya nchi 100. Ripoti inasema homa hiyo sasa inasambaa hata katika maeneo ambayo awali hayakuwa yameathirika.

Kila mwaka maelfu ya watu wanakumbwa na homa hiyo ikiwemo vifo zaisi ya 20,000 huku wengine zaidi ya 264 wakisalia na ulemavu ambao unawalazimisha kubadili mfumo wa maisha yao. Dr Raman Velayudhan ni mtaalamu wa sayansi wa WHO kitengo cha kudhibiti maradhi yanayopuuzwa.

(SAUTI YA DR RAMAN VELAYUDHAN)