Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali zakutana Bangkok kujiandaa kwa mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Doha:UNFCCC

Serikali zakutana Bangkok kujiandaa kwa mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Doha:UNFCCC

Wawakilishi wa serikali kutoka kote duniani wameanza kukutana katika mji wa Bangkok ili kujiandaa kwa ajili ya maazimio yatakayofikiwa kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa utakaofanyika mjini Doha, Qatar.

Kwa mujibu wa msimamizi wa mpango wa mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa (UNFCCC) Christiana Figueres, serikali zimeahidi kupunguza gesi za greenhouse na kuwasaidia watu maskini na walio katika hatari zaidi ya kuathiriwa kuweza kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Amesema serikali zinafahamu kuwa zinahitaji kutekeleza ahadi hizi kikamilifu na kuongeza juhudi zao kabla ya 2020, na hata maradufu zaidi baada ya hapo, na kudhihirisha utekelezaji huo kwenye mkutano wa Doha kwa kuzindua kasi mpya kwa kuafikia mkataba mpya wa kimataifa kuhusu hali ya hewa ifikapo mwaka 2015. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKNDI)