UM yazileta pamoja Israel, Lebanon kujadilia mzozo wa mpakani

30 Agosti 2012

Maafisa kutoka Israel na Lebanon wamekutana kwa majadiliano ya utanzuaji wa hali ya shaka shaka ya mpaka ambayo yanatishia kudumaza hali ya usalama kwa upande zote mbili.

Chini ya upatanishi wa Umoja wa Mataifa pande zote mbili zimeanzisha majadiliano hayo ambayo kimsingi yanafanyika kwa ajili ya kuepusha hali kutoaminiana kama ilivyoshuhudia hapo awali kiasi cha kila upande kutoa matamshi ya tishio/

Mkuu wa vikosi vya ulinzi wa amani vya Umoja wa Mataifa Major General Paola Serra,alikutana na ujumbe wa pande zote mbili kujadilia namna ya utekelezaji wa azimio la Umoja wa Mataifa.

Pande zote zimearifu utayari wa kutekeleza mapendekezo ya baraza la usalama na zimehaidi kuuendelea kuunga mkono ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaopatanisha mzozo huo wa mpaka.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter