Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iran ina wajibu muhimu wa kutekeleza katika eneo la Mashariki ya Kati:Ban

Iran ina wajibu muhimu wa kutekeleza katika eneo la Mashariki ya Kati:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema kuwa Iran ina fursa ya kutekeleza wajibu muhimu katika kanda ya Mashariki ya Kati na katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimataifa.

Bwana Ban ambaye yuko ziarani nchini Iran, ametoa ujumbe wa hongera kwa serikali ya Iran kwa kufanywa mwenyekiti wa jumuiya ya mataifa yasoegemea upande wowote, na kusema kuwa anatazamia kukutana na kufanya mazungumzo muhimu na viongozi wa Iran, pamoja na kuiga mengi zaidi kuhusu utamaduni na historia ya Iran.

Katibu Mkuu amesema Iran in nafasi muhimu hasa zaidi ya kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuutatua mzozo wa Syria, na kusema kuwa atalijadili hili na Kiongozi Mkuu wa kidini, pamoja na rais na viongozi wengine.