Idadi ya wakimbizi wa Afghanistan wanaorejea nyumbani yaongezeka

29 Agosti 2012

Idadi ya wakimbizi wa Afghanistan waliorejea nyumbani kwa kipindi cha miezi minane ya kwanza ya mwaka 2012 kutoka Pakistan, Iran na nchi zingine imepita wakimbizi 50,000. Takariban wakimbizi 213 wamekuwa wakirejea Afghanistan kila siku ikiwa ni ongezeko la asilimia 12 wakati kama huo mwaka uliopita ambapo wakimbizi 190 walikuwa wakirejea nyumbani kila siku.

Wakimbizi 40,000 kati ya wanaorudi nyumbani ni kutoka Pakistan ikiwa ni ongezeko la asilimia 24 ikilinganishwa na mwaka uliopita ambapo wakimbizi 32 ,000 walirejea nyumbani kutoka Pakistan. Wengi wa wakimbizi wanaorejea nyumbani kutoka Pakistan wanalalamikia kupanda kwa gharama ya maisha hasa bei ya vyakula na mafuta. Hata hivyo kurejea nyumbani kwa wakimbizi kutoka Iran kunaonekana kuwa chini hususan kutoka na maisha nafuu ikilinganishwa na Afghanistan hata kama bado kuna wakimbizi milioni moja kutoka Afghanistan walio nchini Iran.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter