Washiriki wa 'Myfishbowl' wachangisha chakula kwa watoto wa shule nchini Lao

29 Agosti 2012

Mchezo “MyFishBowl” ambao ni wa kichina kwenye mtandao wa Facebook umezindua kampeni ya mtandao ya juma moja inayojulikana kama “Hatua Dhidi ya Njaa” kwa ushirikiano na shirika la mpango wa chakula duniani WFP. Kwa siku Moja washiriki kwenye mchezo huo walichangisha zaidi ya dola 100,000 zinazoweza kuwalisha watoto 300,000 wa shule walio kwenye mpango wa WFP wa kutoa chakula shuleni.

Kwenye mchezo huo washiriki wanajaza maeneo yao na samaki ambapo kila mshiriki ananunua samaki kwa dola mbili ambazo huliwezesha shirika la WFP kuwahakikishia kila watoto sita chakula. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter