Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa UM wazindua mkakati wa viwango wastani vya kimataifa vya kudhibiti silaha ndogondogo

Mkutano wa UM wazindua mkakati wa viwango wastani vya kimataifa vya kudhibiti silaha ndogondogo

Mkutano wa wiki mbili unaorejelea mpango wa kuchukua hatua kuhusu silaha ndogondogo haramu umeingia siku yake ya tatu, ambapo imefanyika hafla ya uzinduzi wa viwango wastani vya kimataifa vya kudhibiti silaha ndogondogo. Kikao cha leo pia kimeangazia ufuatiliaji wa usambazaji wa silaha haramu na jinsi ya kukabiliana na athari za silaha hizo, pamoja na takwimu za vifo hasa vya wanawake kutokana na silaha ndogo.

Akifungua mkutano huo mapema wiki hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, alitoa wito kwa serikali kote duniani kufanya juhudi zaidi ili kukomesha usambazaji wa silaha ndogondogo haramu, akitaja silaha hizo kuwa zenye kupendelewa na wale wanaotaka kuasi uongozi wa kisheria, kueneza hofu na kuzorotesha usalama, pamoja na kuyafikia malengo ya kihalifu.

Maeneo ya Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika ni baadhi ya maeneo yaloathiriwa zaidi na usambazaji na utumiaji wa silaha ndogondogo haramu. Mmoja wa wale wanaohudhuria mkutano huo wa wiki mbili ni David Kimaiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Silaha ndogondogo haramu katika ofisi ya rais nchini Kenya.

(SAUTI YA DAVID KIMAIYO)