Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yataka kulindwa kwa sehemu za kitamaduni nchini Libya

UNESCO yataka kulindwa kwa sehemu za kitamaduni nchini Libya

Mkuu wa shirika la elimu sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Irina Bokova amesema kuwa uharibifu wa maeneo ya kitamaduni unaondelea nchini Libya hautakubalika. Bokova ameelezea wasi wasi wake kutoka na uvamizi kwenye maeneo haya akisisitiza kuwa uvamizi huu ni lazima ukomeshwe ikiwa Libya inahitajika kukamilisha mabadiliko kuekea demokrasia.

Kulingana na vyombo vya habari makundi ya kiislamu yalivamia maeneo ya dhehebu la Sufi yakiwemo maktaba kwenye mji ulio kaskazini magharibi wa Zliten pamoja na mji mkuu Tripoli. Bokova ametoa wito kwa utawala nchini Libya kuchukua hatua za kulinda utamaduni na maeneo ya kitamaduni kwa vizazi vichavyo.