Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa UM nchini Somalia wapongeza kuchaguliwa kwa Spika wa Bunge

Ujumbe wa UM nchini Somalia wapongeza kuchaguliwa kwa Spika wa Bunge

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia umepongeza kuchanguliwa kwa spika mpya wa bunge nchini humo ukiutaja kama hatua kubwa kwa taifa hilo ambalo limekumbwa na vita vya muda mrefu. Professor Mohammed Osman Jawari alichaguliwa kwa wingi kwenye uchaguzi uliofanyika katika kituo cha kuwapa mafunzo polisi mjini Mogadishu ambapo watu 230 walishirki.

Mjumbe wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga amesema wabunge nchini Somalia wamepiga hatua muhimu katika kurejesha uwajibika. Amesema kuwa hatua hiyo imeweka msingi kwenye shughuli ya kumchagua manaibu wa Spika na baadaye kufuatiwa na shughuli ya kumchagua rais wa taifa hilo la pembe ya Afrika. Baada ya miongo kadha ya vita Somalia imekuwa kwenye mchakato wa kutafuta amani kupitia kwa mpango unaojulikana kama barabara ya amani.