UM walaani mauaji kwenye eneo la Masisi nchini DRC

29 Agosti 2012

Makundi ya waasi yanaripotiwa kuwaua raia kadhaa na kuwalazimu wengine kuhama makwao tangu mwanzo wa mwezi huu wa Agosti kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo. Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa makundi hayo yaliyojihami yaliendesha uvamizi wa kikatili kwa raia uvamizi ambao umetajwa kuwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu yakiwemo mauaji ya halaiki, uharibifu na uporaji wa mali na kuwalazimu maelfu ya watu kuhama makwao.

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay anasema kuwa uchunguzi unaonyesha kuwa watu kadha wengi wakiwa ni wanawake na watoto waliuawa na waasi. Mkuu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini DRC Scott Campbell anasema kuwa zaidi ya mashambulizi 45 kwenye vijiji 35 na miji yameripotiwa kwenye eneo la masisi mkoani Kivu Kaskazini.

(SAUTI YA SCOTT  CAMPBELL)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud