Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aelekea Iran kuhudhuria mkutano wa NAM

Ban aelekea Iran kuhudhuria mkutano wa NAM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameondoka mjini New York kuelekea mji mkuu wa Iran Tehran ambako anatazamia kuhudhuria mkutano wa jumuiya isiyofungamana na upande wowote

Kandoni mwa mkutano huo wa wiki moja, Ban anatazamia kukutana na viongozi wa mataifa yanayochipukia kiuchumi kwa ajili ya majadiliano katika maaeneo mbalimbali ikiwemo ufuatiliaji maamuzi yaliyofikiwa kwenye kongamano la kimataifa la mazingira Rio+20.

Kwa mujibu wa msemaji wa Katibu huyo Mkuu, Ban anatazamiwa kurejea New York hapo siku ya jumamosi.

Jumuiya hiyo isiyofungamano na upande wowote iliasisiwa mnamo mwaka 1961 wakati wa vuguvugu la vita baridi.Ikiwa na wanachama wapatao 120, NAM sasa inachukua jukumu la kushagihisha masuala ya kimaendeleo kwa nchi wanachama.