29 Agosti 2012
Leo michezo ya olimpiki ya walemavu imefunguliwa rasmi mjini London Uingereza kwa washiriki zaidi ya 4200 kutoka nchi 166 wakishindana katika michezo 21.
Kwa mtazamo wa Umoja wa Mataifa michezo ya olimpiki ya walemavu ni michezo inayotoa fursa muhimu ya kujumuisha wote na kuwawezesha watu wenye ulemavu kupitia michezo na pia ni kusherehekea kuishi kwa amani. Tangu kuanzishwa kwa michezo hiyo baada ya vita ya pili ya dunia michezo ya olimpiki ya walemavu daraja la kuendeleza haki za watu wenye ulemavu, kujumuishwa kwao katika jamii na kuwezeshwa, na mashindano ya mwaka huu hayana tofauti. George Njogopa anaarifu.
(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)