Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO katika jitihada za kuangamiza minyoo ya Guinea

WHO katika jitihada za kuangamiza minyoo ya Guinea

Shirika la afya duniani WHO linafanya jitihada za kukabiliana na minyo ya Guinea baada ya visa 396 vya ugonjwa huo kuripotiwa kwa muda wa miezi sita ya kwanza ya mwaka huu na asilimia kubwa ya visa hivyo ikiripotiwa nchini Sudan kusini huku visa 2 vya ugonjwa huo vikiripotiwa nchini Mali, Chad kisa kimoja na nchini Ethiopia visa 2.

Sudan Kusini imeahidi kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo ifikapo mwaka 2012 hata kama hakuna dawa kamili au chanjo kwa ugonjwa huo. Daktari Gautam Biswas ni kutoka kitengo cha WHO kinachohusika na magonjwa yaliyosahaulika.

(SAUTI YA DR GATAM BISWAS)