Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bado watu milioni 18 wanakabiliwa na uhaba wa chakula Sahel

Bado watu milioni 18 wanakabiliwa na uhaba wa chakula Sahel

Eneo la Sahel magharaibi mwa afrika bado linapitia hali ngumu wakati watu milioni 18 wakiwa wanakabiliwa na uhaba wa chakula kwa mujibu wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF.

Watoto milioni 4 walio chini ya miaka mitano kwa sasa wanakabiliwa na utapiamlo. Nchini Mali ukame na ukosefu wa usalama vimewalazimu zaidi ya watu 435,000 kukimbia makwao wengi wakiwa ni watoto. UNICEF inasema kuwa kati ya hatari zinazokabili eneo hilo ni uvamizi wa nzige na huenda watu milioni 15 wakaathiriwa . Pia visa vya magonjwa ya kipindupindu ni kati ya changamoto zinazoliandama eneo hilo.