Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani mauaji ya mfanyikazi wake nchini Somalia

UM walaani mauaji ya mfanyikazi wake nchini Somalia

Umoja wa Mataifa umelaani maauaji ya mfanyikazi wa shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Matifa FAO kwenye eneo la Marka kusini mwa Somali. Tangu Agosti mwaka 2011 watoa huduma za kibinadamu 20 wameuawa nchini Somalia wanapojitahidi kutoa huduma kwa mamilioni ya watu wanaoteseka nchini humo. Idadi ya raia wa Somalia wanaopokea misaada imeongezeka mara dufu tangu kutangazwa njaa nchini humo mwezi Julai mwaka 2011 ambapo mashirika ya kutoa huduma za binadamu yalifanya jitihada za kuwafikia walioathitika. Umoja wa Matiaifa unatoa wito kwa pande zote nchini Somalia kuruhusu watoa huduma za kibinadamu kuwahudumia wanaotaabika nchini humo popote walipo.