Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wasio na wazazi kutoka Syria wanazidi kukimbilia usalama nchi majirani

Watoto wasio na wazazi kutoka Syria wanazidi kukimbilia usalama nchi majirani

Mzozo unaoendelea nchini Syria umewalazimu mamia ya watoto wasio na wazazi kukimbilia usalama kwenye nchi majirani kwa mujibu wa mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa. Watoto wanaopokelewa na shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa mataifa UNHCR kwenye kambi ya Za’atri nchini Jordan wanasema kuwa wazazi wao wamekufa au wamebaki nyuma kuwatunza wengine na watajiunga nao baadaye.

UNHCR ina hofu kwamba idadi ya watoto wasio na wazazi huenda ikaongezeka na wengi wa watoto wanaonyesha dalili za mshutuko baada ya kutembea kwenye maeneo yaliyo na mizozo bila ya usalama wowote. Patrick McCormick kutoka shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF anasema kuwa maeneo salama kwa watoto yanatengwa kwenye kambi ili kuwapa makao watoto wasio na wazazi.

(SAUTI YA PATRICK MCCORMICK)