Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa UM kuzuru Honduras kuchunguza uzalishaji watoto

Mtaalamu wa UM kuzuru Honduras kuchunguza uzalishaji watoto

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na ustawi wa watoto katika maeneo ya ngono, Najat Maala M’jid anatazamia kufanya ziara yake ya kwanza nchini Honduras kuchunguza madai ya uuzwaji watoto, pamoja na kutumikishwa kwenye vitendo vya ngono.

Ziara hiyo inayotazamiwa kuanza August 30 hadi Septemba 7 inakuja kufuatia mwaliko uliotolewa na serikali ya Honduras ambayo imedhamiria kufanya kazi na mtaalamu huyo kubainisha vyanzo vinavyosababisha maisha ya karaha kwa watoto hao.

Katika ziara yake hiyo anatazamiwa kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Tegucigalpa, La Ceiba na San Pedro Sula. Akiwa huko atakutana na maafisa wa serikali, mashirika ya kiraia na wanaharakati wa masuala ya watoto.