IOM yaanzisha tamasha kuelimisha uhamiaji haramu Ethiopia

28 Agosti 2012

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM likishirikiana na serikali za majimbo nchini Ethiopia imeanzisha tamasha lililopewa dhima ya Mutach yaani yule aliyepotea kwa shabaha ya kutoa elimu inayoelezea athari za kuwepo kwa wahamiaji haramu katika maeneo ya vijijini.

Tayari tamasha hilo limeanzishwa kwenye maeneo ya vijijini na linatazamiwa kudumu hadi mwezi Octoba mwaka huu.Tamasha hilo ambalo linaendeshwa kwa lugha tatu, Oromifa, Tigrigna na Amharic,linatazamia kuwafikia zaidi ya watu 50,000.

Pia tamasha hilo litaendeshwa katika maeneo wanakokutikana wakimbizi kutoka Eritrea waliowekewa makambi katika eneo la Kaskazini mwa Ethiopia.

Tangu kuanzia mwezi March mwaka hu, IOM imewafundisha kiasi cha watu 500 kwa ajili ya kutoa elimu rika na masuala ya kijamii.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter