Global Fund yaidhinisha dola milioni 400 za misaada mipya

28 Agosti 2012

Halmashauri ya mfuko wa ufadhili wa kimataifa katika kukabiliana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria, Global Fund, imeidhinisha maombi 45 mapya ya ufadhili kutoka kwa nchi 37 kwa muda wa miaka miwili. Fedha hizo, jumla ya dola milioni 419.2, zinatarajiwa kufadhili miradi ya kuzuia, kutibu na huduma za uuguzi kwa watu walioathiriwa na magonjwa hayo matatu.

Maombi mengine 11 yenye gharama ya dola milioni 91.2 yalirejeshewa nchi zilizoyatuma ili yarekebishwe, na yanatarajiwa kukaguliwa tena na wataalam huru kabla ya kuidhinishwa.

Meneja Mkuu wa mfuko wa Global Fund, Gabriel Jaramillo, amesema ufadhili huu utahakikisha kuna huduma za kuokoa maisha watu wengi wasioweza kuhesabika kwa urahisi.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter