Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tufani Isaac imedhihirisha haja ya kufunga makambi Haiti:IOM

Tufani Isaac imedhihirisha haja ya kufunga makambi Haiti:IOM

Tufaini Isaac iliyokumba Haiti mwishoni mwa wiki imedhihirisha haja ya kuyafunga makambi 575 yaliyosalia nchini humo tangu tetemeko la ardhi la mwaka 2010, na kutoa huduma ya makazi bora kwa watu 390,000 ambao bado wanaishi kwenye mahema.

Kwa mujibu wa Luca Dall’Oglio mkuu wa mpango wa msaada wa IOM Haiti makambi hayo yamenusurika safari hii lakini wakati ujao yanaweza yasibahatike, na amesema jumuiya ya kimataifa inahitaji kuchukua hatua sasa ya kufunga makambi yote kwa kutoa ruzuku ya kodi za nyumba na suluhu ya makazi kwa wanaoishi kwenye kambi hizo. IOM inasema watu walihamishwa kwenye makambi kabla tufani Isaac haijakumba Haiti na wakarejeshwa tena baada ya tufani kupita. Jean Philippe Chauzy ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JEAN PHILIPPE CHAUZY)