Ripoti ya UM kuhusu Gaza yasisitiza umuhimu wa kuondoa vikwazo

27 Agosti 2012

Umoja wa Mataifa umesisitiza umuhimu wa kuondoka vikwazo na vizuizi dhidi ya Ukanda wa Gaza, ili kupunguza mateso na hali ngumu ya maisha kwa Wapalestina.

Katika ripoti yake inayohoji ikiwa hali ya ukanda wa Gaza itaendelea kuwepo mwaka 2020, wawakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, na Ofisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, wamesema kuwa Ukanda wa Gaza utakabiliwa na maafa mengi ifikapo mwaka 2020, ikiwa vizuizi vilivyoko sasa havitaondolewa.

Kwa mujibu wa mashirika hayo, idadi ya wakazi wa Gaza inatarajiwa kuongezeka hadi zaidi ya watu milioni 2 ifikapo mwaka 2020, huku watu hao wakiendelea kukumbwa na matatizo mengi, yakiwemo watoto kuwa katika hali ya hatari, uhaba wa maji na gharama kubwa ya kununua maji, ukosefu wa nguvu za umeme, uhaba wa wahudumu wa afya na ukosefu wa ajira kwa vijana. Maxwell Gaylard ni afisa wa OCHA katika maeneo yanayokaliwa na Wapalestina.

(SAUTI YA MAXWELL GAYLARD)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter