Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watoa ombi la dola milioni 54 kugharamaia mahitaji kwa wakimbizi wa Syria

UM watoa ombi la dola milioni 54 kugharamaia mahitaji kwa wakimbizi wa Syria

Umoja wa Mataifa umetoa ombi la dola milioni 54 ili kugharamia mahitaji yanayoongezeka kwa maelfu ya wakimbizi wa Syria nchini Jordan, hasa kwa watoto. Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF linasema kuwa fedha hizo zinahitajika kwa dharura kugharamia huduma za afya na za usafi na maji kwa wakimbizi wanaoendelea kuwasili nchini Jordan.

Kwa sasa Jordan ni makao kwa karibu wakimbizi 200,000 kutoka Syria, 17,000 kati yao wakiwa kwenye kambi inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa ya Zaatari huku nusu yao wakiwa ni watoto. UNICEF inasema kuwa hali kwenye kambi ya Zaatari ni mbaya. Viwango vya joto ni vya juu na pia kunashuhudiwa vimbunga vya mchanga vya mara kwa mara.

Umoja wa Mataifa unaonya kuwa wakati idadi ya watoto inazidi kuongezeka ndipo hatari ya mikurupuko ya magonjwa inapozidi kuongezeka pia. Watoto 35,000 wanatarajiwa kwenye kambi hiyo majuma machache