Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wafanya maadhimisho ya kwanza tangu shambulizi kwenye makao yake Abuja, Nigeria

UM wafanya maadhimisho ya kwanza tangu shambulizi kwenye makao yake Abuja, Nigeria

Umoja wa Mataifa nchini Nigeria umefanya maadhimisho ya kwanza kabisa tangu kutokea kwa shambulizi la bomu kwenye makao yake mjini Abuja, ukisema kuwa shambulizi hilo halitozuia Umoja wa Mataifa kutekeleza wajibu wake nchini humo.

Watu 23, wakiwemo wafanyikazi 13 wa Umoja wa Mataifa na 10 wasiokuwa wafanyikazi, waliuawa huku zaidi ya watu wengine 120 wakijeruhiwa. Kwenye hotuba yake mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Nigeria Daouda Toure amepongeza wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa kutokana na moyo ambao wameonyesha tangu kutokea kwa shambulizi hilo.

Toure amesema hata kama shabulizi hilo liligharimu maisha ya wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa na kuwajeruhi watu wengi waliokuwa kwenye jengo lilishambuliwa kwa shughuli mbali mbali za kutoa huduma kwa watu bado hawajatetereka.