Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa UM nchini Somalia wataka shughuli ya kuwachagua mabunge wapya

Ujumbe wa UM nchini Somalia wataka shughuli ya kuwachagua mabunge wapya

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia umeelezea wasi wasi wake kufutia kuendelea kucheleshwa kukamilishwa kwa orodha ya wabunge wapya ukionya kuwa huenda hali hilo ikavuruga mipango ya uchaguzi.

Baada ya miaka mingi ya vita Somalia imekuwa kwenye mchakato wa kutafuta amani ambapo serikali ya mpito ilitekeleza kinachojulikana kama barabara ya amani. Kati ya hatua zilizochukuliwa kumaliza kipindi cha mpito ni pamoja na kuandikwa kwa katiba mpya pamoja na kuchaguliwa kwa wabunge wapya shughuli iliyoendeshwa na wazee 135 wa jadi. Mjumbe wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga amesema kuwa kuzinduliwa kwa bunge jipya la Somalia ni jibu kwa kilichosubiriwa kwa muda mrefu ambacho ni kukamilika kwa kipindi cha mpito kwenye taifa hilo la pembe ya Afrika.