Wajumbe wa fuko la UM juu ya mabadiliko ya tabia nchi wakutana kwa mara ya kwanza

24 Agosti 2012

Mpango wa Umoja wa Mataifa ulioanzishwa kwa ajili ya kukusanya rasilimali zitakazowezesha kurahisisha juhudi za kukabili changamoto za mabadiliko ya tabia nchi umeanzisha mkutano wake wa kwanza.

Mpango huo uliasisiwa mwaka 2011 wakati wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya mazingira na maendeleo huko Durban, Afrika Kusin unashabaha ya kuzisaidia nchi zinazoendelea kukabiliana vyema na changamoto za hali ya joto na mabadiliko ya tabia nchi.

Ilikuwa vigumu kwa mpango huo kuanzisha kikao chake cha kwanza mpaka pale ulipofaulu kujaza nafasi 24 za bodi ya wajumbe ambao kwa msingi ndiyo wanaoratibu na kuongoza fuko la mpango huo.

Bodi hiyo ilizinduliwa kwa kuchaguliwa Bwana Zaheer Fakir kutoka Afrika Kusin na Bwana Ewen McDonald wa Australia kuwa wenyeviti kwa kipindi cha mwaka mmoja.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud