Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaanda mkutano kuhusu uhamiaji kusini mwa Afrika nchini Mauritius

IOM yaanda mkutano kuhusu uhamiaji kusini mwa Afrika nchini Mauritius

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM na ofisi inayohusika na uhamiaji na maendeleo nchini Mauritius wanatarajiwa kuandaa mkutano kuhusu uhamiaji kwenye nchi za kusini mwa Afrika wenye lengo kuunga mkono uhamiaji kwa minajili ya maendeleo ya kuchumi na kijamii kwenye nchi za SADC.

Mkutano huo wa siku mbili ambao inaong’oa nanga Agosti 27 mjini Balaclava nchini Mauritius utawaleta pamoja makatibu wa wizara kutoka nchi za SADC kujadili njia za kunufaika na uhamiaji kati eneo hilo. Mkutano huo utangazia masuala yakiwemo kubuniwa kwa mikakati na sera katika usimamizi wa uhamiaji kwenye nchi za SADC.