Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na washirika wajiandaa kutoa misaada wakati tufani Isaac inapoelekea Haiti

UM na washirika wajiandaa kutoa misaada wakati tufani Isaac inapoelekea Haiti

Serikali imeyaomba mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika wao wajiandae kukabiliana na athari za tufani Isaac. Mashirika la Umoja wa Mataifa na washirika wameanzisha shughuli ya kuhamisha bidhaa za misaada nchini Haiti kwenyewe na kutoka nchini Panama.

Kati ya bidhaa hizo ni pamoja na chakula kinachoweza kuwalisha watu 35,000, vifaa vya kutoa makao na bidhaa zingine za kiafya na za kutibu ugonjwa wa kipindupindu kwa watu 35,000. Nalo shirika la mpango wa chakula duniani WFP limejiandaa na liko tayari kutoa huduma ikiwa litahitajika kufanya hivyo. Tufani hiyo inatarajiwa kuathiri nchini tatu zikiwemo Haiti, Jamhuri ya Dominica na Cuba. Inakadiriwa kuwa huenda watu 500,000 wakaathiriwa na tufani hiyo wakiwemo wakimbizi wa ndani 300,000. Jens Learke ni msemaji wa OCHA.

(SAUTI YA JENS LEARKE)