Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shughuli za kuwasaidia wakimbizi kutoka Syria zaanza:UNHCR

Shughuli za kuwasaidia wakimbizi kutoka Syria zaanza:UNHCR

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa kuendelea kuzoroteka kwa hali ya usalama nchini Lebanon kunazuia oparesheni zake. Wakimbizi wanaendelea kuingia nchini Lebanon hasa kutoka miji ya Damascus, Aleppo na Daraa huku kukiwa na karibu wakimbizi 51,000 kutoka Syria nchini Lebanon waliotuma maombi au waliojiandikisha na UNHCR.

Wakimbizi 74,000 tayari wameandikishwa nchini Uturuki huku wakimbizi 61,000 wakiwa wameandishwa nchini Jordan. Nchini Iraq wakimbizi 15,898 kutoka Syria wameandikishwa. Kwa ujumla kuna raia wa Syria 202,512 waliovuka mpaka na kujiandikisha na UNHCR kwenye nchi majirani. Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)