Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Filamu kuhusu utunzi wa maji yazinduliwa

Filamu kuhusu utunzi wa maji yazinduliwa

Shirika la Elimu Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO na wizara ya mazingira nchini Korea Kusini wana mipango ya kuweka filamu fupi kwenye mtandao kuhusu upatikanaji wa maji safi na mazingira safi yenye lengo la kuweka sera kuhusu usimamizi wa maji na pia kutoa hamasisho kuhusu masuala ya maji.

Maji ni muhimu kwa afya ya binadamu lakini hata hivyo katika sehemu nyingi za ulimwengu maji si salama kwa matumizi ya binadamu. Filamu hiyo itaangazia matatizo ya maji yakiwemo upatikanaji wa maji safi na usafi, uchafuzi wa maji na hatari zinazokumba maji. Filamu hiyo ilizinduliwa rasmi kwenye kongamano la sita kuhusu maji mjini Marseille machi mwaka 2012 na inatarajiwa kuonyeshwa kwenye warsha za maji za kimataifa.