Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Naibu Katibu Mkuu wa UM asisitiza umuhimu wa kutatua mizozo kwa njia ya amani

Naibu Katibu Mkuu wa UM asisitiza umuhimu wa kutatua mizozo kwa njia ya amani

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amesisitiza umuhimu wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa katika kutatua migogoro kwa njia ya amani

Mwanadiplomasia huyo kutoka Uswiss amesema sehemu za mkataba anazofurahia zaidi ni sura mbili. Moja ni sura ya VI ambayo inahusika na kutuatua mizozo kwa njia ya amani na sura ya VII ambayo inapendekeza mipango ya kikanda ili kusuluhisha migogoro. Akizungumza na Maha Fayek wa Radio ya UM bwana Eliasson amesema kuwa katika maisha na siasa ni muhimu kuweka na kufwata baadhi ya kanuni na maadili.

(SAUTI YA JAN ELIASSON)