Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utafiti mpya wachunguza jinsi shule zinavyofundisha historia ya mauaji ya kimbari ya wayahudi ya Holocaust

Utafiti mpya wachunguza jinsi shule zinavyofundisha historia ya mauaji ya kimbari ya wayahudi ya Holocaust

Ni vipi shule kote duniani zinafundisha suala la Holocaust, yaani mauaji ya kimbari ya wayahudi wanaokadiriwa kuwa milioni sita, yalotekelezwa na serikali ya Adolf Hitler? Na ni katika maeneo yapi duniani kunakofundishwa historia ya Holocaust?

Majibu kwa maswali haya yanatarajiwa kupatikana kutokana na mradi unaosimamiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO, likishirikiana na Taasisi ya Georg Eckert Institute for International Textbook Research. Mradi huo unaoitwa ‘hali ya kimataifa ya elimu kuhusu Holocaust’, utawezesha kwa mwara ya kwanza kulinganisha jinsi suala la Holocaust linavyofundishwa katika shule na katika mifumo ya elimu ya kitaifa kote ulimwenguni.

Mradi huo wa miezi 18, utaanza kwa kuchunguza utaratibu wa masomo kutoka nchi 195, ukionyesha ni wapi na ni kwa kiwango gani suala la Holocaust limewekwa katika utaratibu rasmi wa masomo ya shule. Matokeo yake yataonyesha ni wapi linafundishwa suala hilo, na jinsi gani linafundishwa.