Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa UM aitaka Marekani kufanya mazungumzo na watu wa asili kuhusu uuzaji wa ardhi

Mtaalamu wa UM aitaka Marekani kufanya mazungumzo na watu wa asili kuhusu uuzaji wa ardhi

Mtaalamu huru kutoka Umoja wa mataifa ametoa wito kwa serikali ya Marekani na utawala kwenye jimbo la South Dakota kuanza mazungumzo na watu wa asili kuhusu suala la uuzaji wa ardhi ambao huenda ukaathiri eneo lenye umuhimu kwa kidini kwao.

Mjumbe huyo maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za jamii za kiasili James Anaya anasema kuwa ardhi hiyo ya ekari tano iliyo kati ya watu wa Lakota, Dakota na Nakota imetangazwa kuuzwa mwishoni mwa wiki hii. Kulingana na Anaya watu hao wana hofu kuwa kuuzwa kwa ardhi hiyo huenda kukasababisha wao kuzuia kuingia eneo hilo kwa shughuli zao za kidini.