Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muafaka wa mataifa mawili huru ndilo suluhisho pekee kwa mzozo wa Israel na Palestina:UM

Muafaka wa mataifa mawili huru ndilo suluhisho pekee kwa mzozo wa Israel na Palestina:UM

Licha ya kuwepo mkwamo katika mazungumzo kati ya Waisraeli na Wapalestina, muafaka wa mataifa mawili huru bado ndio suluhu inayofaa, amesema mkuu mpya wa masuala ya kisiasa wa Umoja wa Mataifa, Jeffrey Feltman, wakati akilihutubia Baraza la Usalama siku ya Jumatano.

Bwana Feltman amesema kuwa Umoja wa Mataifa unaamini kuwa pande hizo mbili, pamoja na nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa, zinapaswa kuzingatia vitendo vyao katika muktadha wa lengo hilo.

Amelikumbusha Baraza la Usalama kwamba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliwaomba viongozi wa kikanda kutumia ushawishi wao kupunguza, badala ya kuchagiza utata zaidi.