Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM nchini Kosovo azitolea mwito jumuiya za kimataifa kulipiga jeki taifa hilo

Mjumbe wa UM nchini Kosovo azitolea mwito jumuiya za kimataifa kulipiga jeki taifa hilo

Mkuu wa ujumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Kosovo amezitolea mwito jumuiya za kimataifa kuchukua hatua mpya juu ya utekelezaji mipango ya kulisaidia taifa hilo.

Farid Zarif amesema kuwa jumuiya za kimataifa zinapaswa kubadilisha makusudio yao kuhusu kulipiga jeki taifa hilo tena akasisitiza kuwa zinapaswa kuonyesha vitendo halisi kwa kuanzisha malengo ya kweli.

Kamishna hiyo ilianzishwa mwaka 1999 kufuatia mapigano makali ya kikabila yaliyohusisha jamii ya waserbia na waalbania huko Kosovo.

Ujumbe huo umekuwa ukifanya kazi kupalilia mazingira ya amani na utulivu kwa wakazi wa eneo hilo na ikihusisha mamlaka toka pande zote zinazohusika