Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bhutan, Columbia, Indonesia na Rwanda zatunukiwa na UNESCO katika masuala ya elimu

Bhutan, Columbia, Indonesia na Rwanda zatunukiwa na UNESCO katika masuala ya elimu

Mipango ya kujua kusoma na kuandika kutoka Bhutan, Indonesia, Colombia na Rwanda ndiyo iloshinda tuzo za UNESCO mwaka 2012. Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova amewatangaza washindi hao leo, ambao walipendekezwa na jopo la majaji wa kimataifa.

Washindi watazipokea tuzo zao kwenye hafla ambayo itafanyika kwenye makao makuu ya UNESCO mnamo tarehe 6 Spetemba, kama sehemu ya shughuli za siku ya kimataifa ya kujua kusoma na kuandika, ambayo huadhimishwa kila Septemba 8.

Halmashauri ya Maendeleo ya Elimu ya Jamii Indonesia itapokea moja ya tuzo za UNESCO za Mfalme Sejong. Kwa mujibu wa UNESCO, mpango huo wa serikali unaohusu kuboresha viwango vya elimu ya kujua kusoma na kuandika kwa kufundisha ujasiriamali, desturi ya kusoma na kutoa mafunzo ya walimu, unahusu takriban watu milioni 3, na unazingatia hususan wanawake wasojua kusoma na kuandika, ambao mbali na kufundishwa kusoma na kuandika, wanafundishwa stadi mbali mbali za maisha. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)