Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Baraza Kuu awapongeza Waislamu kwenye Siku ya Eid Al-Fitr

Rais wa Baraza Kuu awapongeza Waislamu kwenye Siku ya Eid Al-Fitr

Huku Waislamu wakiadhimisha siku ya Eid al-Fitr Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser amewatakia Waisalmu wote heri njema, mali na afya nzuri wanaposheherekea siku hii.

Amesema kuwa sherehe hizo ambazo ni za kuadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhan zinajiri wakati inapoendelea kumalizika kikao cha 66 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa huu ni wakati wa kuombea mamilioni ya watu duniani wanaoteseka wakipitia dhulma za kila aina.

Ameongeza kuwa wakati wa kuadhimisha siku hii ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha kuwepo ushirikiano kukabiliana na changamoto za ulimwengu.