Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi wa kijani utasaidia kutengeza ajira mpya Hispania:ILO

Uchumi wa kijani utasaidia kutengeza ajira mpya Hispania:ILO

Ripoti moja iliyotolewa na taasisi ya kimataifa inayohusika na maendeleo endelevu imesema kuwa Hispania inahitaji kuchukua mkondo sahihi wa kutekeleza mipango inayojali uchumi unaozingatia mazingira hasa katika kipindi hiki ambacho taifa hilo linapitia wakati mgumu wa ongezeko la ukosefu wa ajira.

Ripoti hiyo ambayo ni sehemu pia ya vidokezo vya shirika la kazi duniani ILO imesema kuwa wakati tatizo la ajira kwa vijana likizidi kupanda, Hispania inapaswa sasa kukazania uchumi endelevu tena ule unazingatia mazingira.

Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Hispania kinaarifiwa kupanda hadi kufikia asilimia 50. Lakini ripoti hiyo inasema kuwa iwapo mamlaka za Hispania zitafaulu kuongeza juhudi utekelezaji mipango ya uchumi endelevu, basi inaweza kufaulu kwa kiasi kikubwa kutengeneza ajira mpya.