Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Argentina yatekeleza kwa vitendo mpango wa MERCOSUR na kuwahalalisha wahamiaji zaidi ya milioni

Argentina yatekeleza kwa vitendo mpango wa MERCOSUR na kuwahalalisha wahamiaji zaidi ya milioni

Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na uhamiaji IOM limezindua chapisho lake linaloangaazia mpango unaojulikana MERCOSUR ambayo inalenga kuimarisha ustawi wa watu jamii ya wahamiaji.

Katika chapisho hilo IOM imeeleza pia hatua zilizochukuliw a na serikali ya Argentina ambayo imeuhalalisha mpango huo na kuwafaidia jamii ya wahamiaji milioni kadhaa wanaoshi nchini humo.

Katika kipindi cha mwaka 2004, Argentina iliridhia mpango ilioupa jina Patria Grande ambao uliwalenga makundi ya wahamiaji wanaishi nchini humo kwa ajili ya haki za kiustawi na maingiliano mengine kwenye maeneo ya kiuchumi na kisiasa.

Mataifa kadhaa katika eneo la Amerika ya Kusin ni miongoni mwa nchi zinazotambua mpango huo ambao dhamira yake kubwa ni kuzitaka dola za eneo hilo kuwahalalisha wahamiaji wanaopatikana ndani ya mipaka yao.