Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa UM Syria kuondoka mwishoni mwa juma

Ujumbe wa UM Syria kuondoka mwishoni mwa juma

Wakati ujumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa ukitaraji kusitisha shughuli zake nchini Syria, Baraza la Usalama lilikutana kujadilia hali ya mambo nchini humo limekubali kuanzisha ofisi itayohusika na usaidizi wa kisiasa ambayo pia itamulika masuala ya haki za binadamu.

Umoja wa Mataifa umesema utaondoa ujumbe wake ifikapo jumapili usiku katika wakati hali ya mapigano bado ni ya kiwango cha juu kukishuhudiwa uvamizi katika meneo mengi zaidi.

Kulingana na duru za kidiplomasia Umoja wa Mataifa haungependa kujitoa kabisa kwenye eneo hilo badala yake inaangalia uwezekono kuanzisha wakala maalumu ambaye atasaidia michakato ya kisiasa na kujaribu kuongeza ushawishi kwa pande zote zinazohasimiana.

Tangu kuzuka kwa wimbi la kutaka kuondosha madarakani utawala wa Assad miezi 17 iliyopita inakadiriwa kiasi cha raia 17,000 wamepoteza maisha na wakati huu kunashuhudiwa hali ya mkwamo zaidi.

Kuna ripoti ya kuongezeka kwa machafuko katika Miji miwili muhimu ya Damascas na ule wa Alepp kiasi cha kusababisha raia wengi kuingia uhamishoni na wengine wakisalia bila makazi.