Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yachunguza sheria mpya iliyopitishwa na Australia kuhusu watafuta hifadhi

UNHCR yachunguza sheria mpya iliyopitishwa na Australia kuhusu watafuta hifadhi

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linachunguza mapendekezo yaliyotolewa na taifa la Australa wiki hii kutoka kwa kundi moja la wataalamu na uamuzi ulitolewa na bunge ambapo watafuta hifadhi wataandikishwa kwenye kambi zilizo kwenye bahari ya Pacific. Hata hivyo matakwa ya UNHCR yamesalia kuwa mipango itakayoruhusu watafuta hifadhi wanaowasili kwa mashua nchini Australia kufanywa nchini Australia. Kulingana na UNHCR ni jambo muhimu iwapo mpango wowote unaohusu utoaji wa hifadhi unafuata sheria na pia kutekelezwa na kutetea na kulinda haki za binadamu. UNHCR inasema kuwa ina matumani ya kujadili masusla ya mabadiliko hayo na seriali ya Australia hivi karibuni.