Mashirika ya kibinadamu yalenga kuwasaidia watu milioni 6 nchini Yemen

17 Agosti 2012

Mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu yanalenga kuwahudumia watu milioni sita mwaka huu wa 2012 ikiwa ni ongezeko la asilimia 62 ikilinganishwa na miezi sita iliyopita. Kulingana na makadirio fedha zinazozohitajika kwa sasa ni jumla ya dola milioni 584.

Katika eneo la Abya lililo kusini mwa nchi, shirika la kuratibu masusla ya kibinadamu OCHA limezindua mpango mwingine kufuatia mapigano ya mwezi Mei. Kwa sasa watu 320,000 wanahitaji usaidizi wa dharura kufutia makadirio kuwa mapigano ya mwezi Mei yalisabisha watu 237,000 kuhama makwao huku baadhi yao wakiwa wamerejea nyumbani. Watu hao wanahitaji misaada ya chakula , makao , huduma za afya, usalama , elimu na maji. Jens Laerke ni msemaji wa OCHA.

(SAUTI YA JENS LAERKE)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud