Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasambaza misaada kwa wakimbizi wa ndani nchini Syria

IOM yasambaza misaada kwa wakimbizi wa ndani nchini Syria

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeazisha usambazaji wa misaada isiyokuwa chakula kupitia kwa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kwa watu waliohama makoa ambao kwa sasa wamepiga kambi kwenye shule nne mjini Damascus.

Juma hili IOM ilisambaza vifaa 581 kwa usafi kwenye shule ya Fariz Daboos kwenye shule ya Somaya Al Makhzomiya pamoja na kwenye shule za Adnan Kolaki na Ghaliyah Farahat. Kati ya misaada waliyopokea ni pamoja na sabuni , dawa ya ,meno na vifaa vingine vya usafi. Familia nyingi zinazopiga kambi shuleni zinatoka sehemu tofauti za mji wa Damascus na nyingi zilikimbia baada ya kutokea mapigano karibu na makwao mwezi Julai.