Wakimbizi zaidi wanaendelea kukimbilia nchi jirani kwa sababu ya ghasia Syria:UNHCR

17 Agosti 2012

Kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya raia wa Syria wanaokimbilia Uturuki, limesema Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR. Kati ya Jumanne na Jumatano, watu 3,500 walivuka mpaka na kuingia katika mikoa ya Kilis na Hatay, kwa mujibu wa maafisa wa serikali mikoani.

Watu 1700 waloingia kwenye mkoa wa Kilis walitoka kwenye maeneo ya Azaz na Aleppo, na pia Latakia na Idlib. Kutokana na idadi hii ya wakimbizi wapya, idadi ya wakimbizi wa Syria katika kambi tisa nchini Uturuki imefikia takriban watu 65,000 sasa, ingawa wote hawajaandikishwa. Takriban asilimia 40 ya watu hawa wamewasili mwezi Agosti pekee. George Njogopa na taarifa kamili

(RIPOTI YA GEORGE)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud