Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waadhimisha Siku ya Watoaji Huduma za Kibinadamu duniani

UM waadhimisha Siku ya Watoaji Huduma za Kibinadamu duniani

Kila Agosti 19 ni Siku ya Watoaji wa Huduma za Kibinadamu, na leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, imefanyika hafla ya kuweka ua la heshima kwa kumbukumbu ya wahudumu wa Umoja wa Mataifa ambao waliuawa mjini Baghdad, pamoja na watoaji huduma za kibinadamu wote ambao wameuawa wakijaribu kwa ajili ya kutetea amani

Katika kuadhimisha siku hii, Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakizungumzia umuhimu wa siku yenyewe, na changamoto yanazokumbana nazo. Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP limesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita pekee, wahudumu wake 12, wakiwemo wadau wake wameuawa wakati wakifanya kazi kukabiliana na njaa nchini Somalia, Sudan, Haiti, Sudan Kusini na Ivory Coast. Nalo shirika la Afya Duniani, WHO, limesema utoaji wa huduma za Afya nchini Syria unakabiliwa na changamoto za kiusalama na uhaba wa madawa. Shirika hilo pia limetaja maeneo ya hatari na yanayotia wasiwasi barani Afrika, yakiwemo jimbo la Kivu ya Kaskazini katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, ambako maelfu ya watu wamelazimika kuhama makwao kwa sababu ya machafuko, Somalia na eneo la Sahel.

Ili kufahamu hali halisi ya changamoto wanazokumbana nazo watoa huduma za kibinadamu, nimezungumza na ....