UNHCR yatoa ushauri kwa wakimbizi kutoka Bhutan walio nchini Nepal

16 Agosti 2012

Prem Bahadur mwenye umri wa miaka 25 ana matumani ya kupata makao mapya kwa kuwa anaelewa kuwa kuna huduma nzuri kwenye nchi zinazowachukua watu walio na matatizo ya kuona.

Lakini hata hivyo babake mwenye umri wa miaka 60 ana hofu kuwa huenda mwanawe akakumbwa na matatizo ya kuishi kwenye nchi mpya kutokana na tatizo lake la kutoona. Hata baada ya zaidi ya wakimbizi 69,000 kutoka Bhutan walio kwenye kambi nchini Nepal kupewa makao kuna watu kama Prem Bahadur na familia ambazo zimekosa uamuzi iwapo zinahitaji kuhamia nchi tofauti au wasalie kambini wakiwa na matumani ya kurudi Bhutan.

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeanzisha shughuli ya kutoa ushauri kwenye kambi kusaidia familia kupata majibu na kutoa suluhu kwa wakimbizi hawa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter