Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa UM azuru Guatemala kwa sababu ya uuzaji watoto na dhuluma za Kingono

Mtaalamu wa UM azuru Guatemala kwa sababu ya uuzaji watoto na dhuluma za Kingono

Mtaalam wa wa haki za binadamu katika Umoja Mataifa, Najat Maalla M’jid ataizuru nchi ya Guatemala tokea tarehe 20 hadi 29 Agosti mwaka huu. Hii itakuwa ziara ya pili kufanywa na mtaalam huru, tangu ziara ya miwhso iliyoidhinishwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mwaka 2000, ili kuchunguza uuzaji wa watoto, kuhusishwa watoto katika biashara ya ngono na katika video na picha za ngono.

Bi M’jid amesema katika ziara yake ataangazia viwango, mienendo mipya na asili ya suala la uuzaji na kudhulumiwa kwa watoto kingono, na mikakati iliyowekwa ya kuzuia na kulinda watoto dhidi ya kuuzwa na kunyanyaswa kingono. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)